Shirika la Uhamiaji la Kimataifa (IOM) Jumapili limesema boti iliyobeba abiria 350 ilipinduka nje ya pwani ya Djibouti, ambapo wahamiaji wasiopungua 109 wakiwemo watoto 15 wamefariki, na wengine zaidi ya 116 hawajulikani walipo.
Boti hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka Djibouti kuelekea Yemen ilipinduka usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa. Timu za IOM pamoja na mamlaka za huko wako kwenye eneo la tukio kutoa msaada wa dharura. Mkuu wa tume ya IOM nchini Djibouti Alexandre Coissac amesema ajali hiyo ni janga la kuhuzunisha lililosababisha watu wengi kupoteza maisha.
Miili 109 imepatikana, wakiwemo wanaume 52, wanawake 42 na watoto 15. Watu zaidi ya 80 wamenusurika kwenye ajali hiyo. Mamlaka za Djibouti zinaendelea na kazi za utafutaji na uokoaji.
