Tanzania yatuma kampuni 36 kwenye maonyesho ya CIIE ya China

Tanzania imetuma kampuni 36 na taasisi za serikali kwenye Maonyesho ya tisa ya Kimataifa ya Uagizaji ya China (CIIE), yanafanyika kuanzia Novemba 5 hadi 10 mjini Shanghai, China.

Kampuni na taasisi hizo zilitambulishwa kwenye sherehe ya kuagwa iliyoandaliwa mjini Dar es Salaam na Ubalozi wa China nchini Tanzania, ambapo baadhi ya waonyeshaji walionyesha bidhaa zao, ikiwa ni pamoja na kahawa, chai na asali.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania Bw. Dennis Londo alisema maonyesho hayo yanatoa fursa muhimu kwa kampuni za Tanzania kuonyesha bidhaa zao, kuanzisha ushirikiano na kuvutia wawekezaji kutoka China na masoko mengine ya kimataifa.

Balozi wa China nchini Tanzania Bibi Chen Mingjian amesema sera ya ushuru sifuri ya China ni fursa kwa wauzaji nje wa bidhaa wa Tanzania, na kuwa thamani ya uagizaji bidhaa wa China kutoka Tanzania imeongezeka na kufikia dola milioni 290, likiwa ni ongezeko la asilimia 12 kwa mwaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live