IMF yakadiria ukuaji wa asilimia 4.5 kwa Afrika kusini mwa Sahara

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limekadiria kuwa, uchumi wa kanda ya Afrika kusini mwa Sahara unatarajiwa kukua kwa asilimia 4.5 mwaka 2026 na 2027, na kuonya kuwa, kuongezeka kwa mashinikizo ya kiuchumi kunaweza kudhoofisha ufufukaji wa kanda hiyo.

Katika ripoti yake ya hivi karibuni ya makadirio, IMF imesema nchi za kanda hiyo zimeonyesha ustahimilivu kwa kuvurugika kunakohusiana na mgogoro wa Mashariki ya Kati, zikiungwa mkono na marekebisho katika usambazaji wa nishati duniani, mapato yanayotokana na mauzo ya bidhaa katika baadhi ya nchi na mageuzi ya mapema ya kiuchumi.

IMF imeonya kuwa, serikali zina ukomo wa uwezo wa kukabiliana na mishtuko zaidi, kutokana na gharama kubwa za malipo ya madeni, akiba ndogo ya fedha za kigeni na kupungua kwa msaada wa kimataifa.

Pia hali mbaya ya hewa, hususan kuongezeka kwa hali ya hewa ya El Nino, inaleta tishio lingine kubwa kwa uzalishaji wa chakula na upatikanaji wa umeme.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live