China iko tayari kufanya kazi na pande zote kwa ajili ya manufaa ya APEC

China iko tayari kushirikiana na pande zote ili kufanya kazi nzuri katika sehemu ya mwisho wa “Mwaka wa China” wa APEC 2026 na kuchangia kupata matokeo mazuri katika mkutano ujao wa Viongozi wa Uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki (APEC).

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi jana alipoongoza Mkutano wa 37 wa Mawaziri wa APEC kwa njia ya video kwa pamoja na Waziri wa Biashara wa China, Wang Wentao, na kuongeza kuwa, mkutano huo ni muhimu kuhusiana na maendeleo ya baadaye ya kanda ya Asia na Pasifiki.

China itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa APEC utakaofanyika Shenzhen, kusini mwa China mwezi huu, ambapo itakuwa ni mara ya tatu kwa China kuwa mwenyeji wa mkutano huo.

Kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Kujenga Jamii ya Asia na Pasifiki Ili Kustawi kwa Pamoja”, huku China ikitambua uwazi, uvumbuzi na ushirikiano kama maeneo matatu ya kipaumbele kwa ushirikiano wa mwaka huu wa APEC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live