Tarehe 21 Novemba 2026, huko Harbin, mkoani Heilongjiang,China,ikiwa sehemu muhimu ya shughuli za ukuzaji wa utamaduni na utalii zilizoandaliwa na idara ya utamaduni na utalii ya Chaoshan huko Harbin, Ngoma ya jadi ya Yingge ya Chaoshan ilionyeshwa katika Mtaa wa Kati, mtaa wenye historia ya miaka mia moja wa mji wa Harbin na kuvutia wakazi na watalii wengi kusimama na kuitazama.
Yingge ni ngoma ya jadi ya kitamaduni ya eneo la Chaoshan, mkoani Guangdong,China, inayochanganya vipengele mbalimbali kama maigizo, densi na sanaa ya Wushu, na mwaka 2006 ilijumuishwa katika orodha ya kwanza ya kitaifa ya urithi wa utamaduni usioshikika.
