Mkutano wa COP31 uliorefushwa wahitimishwa Uturuki bila kufikia makubaliano

Mkutano wa 31 wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa (COP31) ulimalizika jana Novemba 22 bila makubaliano ya jumla baada ya mazungumzo yake kurefushwa kwa muda wa karibu saa 48.

Mwenyekiti wa COP31 ambaye pia ni waziri wa mazingira, ukuaji wa miji na mabadiliko ya tabianchi wa Uturuki Murat Kurum amesema katika kikao cha kuhitimisha kuwa jukumu la Uturuki kama mwenyekiti litaendelea hata baada ya mkutano huo, akiashiria nishati safi, mipango ya Taka-Sifuri na ufadhili wa tabianchi iliyozinduliwa chini ya ajenda ya utekelezaji ya mkutano huo.

Katibu Mtendaji wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Mabadiliko ya Tabianchi Simon Stiell naye pia anahisi kuvunjika moyo kama wengine kutokana na kushindwa kufikiwa makubaliano ya kina na ya jumla, akibainisha kuwa maamuzi muhimu ya mazungumzo yamefikiwa, yakiwemo mpito wa haki.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema katika taarifa yake kuwa amesikitishwa na matokeo hayo, akitoa wito kwa dunia kujitahidi zaidi kukabiliana na msukosuko wa tabianchi.

COP31 President Murat Kurum walks through the venue for the COP31 U.N. Climate Summit, Sunday, Nov. 22, 2026, in Antalya, Turkey. (AP Photo/Khalil Hamra)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live