Wananchi wa Uganda wapanga foleni kupokea vyandarua vya bure

Wizara ya Afya nchini Uganda imefanya duru ya tano na ya mwisho ya kampeni ya kitaifa ya mwaka 2026 ya usambazaji wa vyandarua vya muda mrefu vyenye dawa ya kuua wadudu katika miji ya Kampala na Wakiso, katikati ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Kudumu wa Wizara ya Afya ya Uganda Dk. Diana Atwiine, vyandarua zaidi ya milioni 3.38 vya muda mrefu vyenye dawa ya kuua wadudu vimesambazwa katika duru hii. Lengo la kampeni ni kufunika kila familia, kufikisha chandarua kimoja kwa kila watu wawili, na kutoa kipaumbele kwa watoto chini ya miaka mitano na wanawake wajawazito. Picha zikionyesha wananchi wakiwa kwenye foleni kuchukua vyandarua vya bure.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live