Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesifu umuhimu wa kimkakati unaozidi kukua wa reli ya Ethiopia-Djibouti, akibainisha kuwa ongezeko kubwa la idadi ya abiria, upanuzi wa uwezo wa uchukuzi, na huduma za ugavi zenye thamani iliyoongezwa vinaleta mabadiliko kwenye biashara ya kikanda. Abiy ametoa kauli hiyo wakati akiwasilisha ripoti ya utendaji wa serikali mbele ya Baraza la Wawakilishi wa Wananchi, ambalo ni baraza la chini la Bunge la Ethiopia. Akizungumzia upanuzi wa huduma za abiria na mizigo za reli hiyo iliyojengwa na China, amebainisha kuwa idadi ya abiria imeongezeka karibu mara tatu, kutoka 198,000 hadi 588,000, na kiasi cha mizigo iliyosafirishwa kimefikia tani milioni 4.3 kwa mwaka.
Reli ya Ethiopia-Djibouti yenye urefu wa kilomita 752, inazidi kuwa njia inayopendelewa zaidi na Ethiopia kwa ajili ya kusafirisha bidhaa zake nje na kuingiza bidhaa kutoka nje. Asilimia zaidi ya 95 ya mauzo ya kahawa ya nchi hiyo katika nchi za nje, pamoja na asilimia 25 ya mbolea inayoingizwa nchini, kwa sasa husafirishwa kwa kutumia reli hii.
