Kampuni ya Sanyi ya China yaonyesha Lori la Mgodi la Umeme linalojiendesha katika Maonyesho ya Mashine za Uhandisi ya Shanghai

Kampuni ya Sanyi kwa mara ya kwanza imeonyesha lori lake la mgodi la umeme linalojiendesha lenye uwezo wa tani mia katika maonyesho ya mashine za uhandisi yaliyofanyika mjini Shanghai,China, lori hilo pia ni la kwanza katika sekta hii kuondoa chumba cha dereva.

Baada ya kuondoa chumba cha dereva, uwiano wa mzigo wa lori hili umeongezeka kwa 12%,na kwa mfumo wake wa chaji,linaweza kuchajiwa kikamilifu ndani ya dakika 35, hivyo kuongeza takriban saa moja ya muda wa kazi kila siku.

Lori hilo limeunganishwa na mfumo wa usimamizi na uratibu wa akili bandia wa Sanyi na linaweza kujiendeshwa chini ya mfumo huo kufanya upakiaji, usafirishaji na upakuaji, na linaweza kufanya kazi katika mazingira ya mtandao hafifu wa Internet.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live