Waokoaji wanaendelea na juhudi za kuwatafuta manusura baada ya maporomoko makubwa ya matope, yaliyosababishwa na maporomoko ya barafu huko Nepal, kugonga forodha ya mpakani ya Gyirong Mkoani Xizang. Serikali ya mkoa huo imesema janga hilo lililotokea Agosti 26, limesababisha vifo vya watu 16, na wengine 546 bado hawajulikani walipo.
Licha ya changamoto ya miinuko mirefu, mabonde makali na hali ngumu ya hewa, waokoaji wanasonga mbele katika eneo la maafa, wakifanya shughuli za kuondoa matope barabarani, utafutaji na uokoaji, utambuzi wa hatari, usafi wa vijidudu na kuzuia milipuko ya magonjwa, pamoja na kusafisha na kurejesha njia zilizoharibika.
Waokoaji huko wamesema eneo la kiini limefunikwa na matope na mawe yaliyosambaa, pamoja mikondo ya maji yenye utatanishi.
