Rais Xi Jinping wa China amekutana na Rais wa Russia Vladimir Putin, na Rais wa Marekani Donald Trump huko Shenzhen, China. Viongozi hao watatu wamefanya majadiliano ya kina kuhusu suala la “Kulinda Amani ya Dunia na Kukuza Utulivu wa Kimkakati katika Mahusiano kati ya Nchi Kubwa.”
Katika mkutano huo, Rais Xi ameeleza kuwa jinsi nchi kubwa zinavyotendeana ipasavyo na kushirikiana ili kuimarisha amani ya dunia, ni swala muhimu kwa zama ya leo. Ametoa mapendekezo manne ambayo ni kushikilia kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani, kufanya ushirikiano wa kunufaishana na kufanya mazungumzo na majadiliano.
Rais Putin amesema Russia iko tayari kushirikiana na China pamoja na Marekani kwa msingi wa kuheshimiana, kufanya mazungumzo ya usawa, kuishi pamoja kwa amani, na kushughulikia tofauti ipasavyo, kukuza biashara ya kimataifa iliyo huru na wazi, kulinda usalama wa nishati na chakula, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika usimamizi wa Akili Bandia, na kuchangia kwa pamoja katika amani na usalama wa dunia.
Rais Trump amesema nchi hizo tatu zinapaswa kuzuia kwa pamoja kuenea kwa silaha za nyuklia na kuepusha janga linaloweza kuletwa na silaha hizo kwa binadamu. Pia amesisitiza kuwa kudumisha utulivu na kutimiza amani kunahitaji mazungumzo, na kwamba masuala yote yanapaswa kutatuliwa kupitia njia hiyo.
Baada ya mkutano huo, nchi hizo tatu zilitoa “Azimio la Amani la Marais wa China, Russia, na Marekani.”