Kenya yaanzisha mpango wa kukabiliana na El Nino ili kulinda mifugo

Kenya imeanzisha mpango wa hatua za mapema kukabiliana na athari za El Nino kwa sekta ya mifugo Alhamisi wiki hii, ukiwa na thamani ya shilingi za Kenya bilioni 2.1 (takriban dola za kimarekani milioni 16.2).

Waziri wa maendeleo ya mifugo na kilimo Bw. Mutahi Kagwe amesisitiza ahadi ya serikali ya kulinda uchumi wa mifugo kwa kuchukua hatua za mapema kabla ya hasara kutokea, akikumbusha athari mbaya zilizosababishwa na El Nino mwaka 2023 na mafuriko ya mwaka 2024, ikiwemo hasara kubwa kwa wafugaji na miundombinu, na mlipuko wa magonjwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live