
Kocha mkuu wa timu ya Uganda Paul Put ametangaza timu ya wachezaji 28 kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) la 2027.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), michuano ya hatua ya makundi itaanza mwezi huu, na kuendelea hadi mwezi Machi mwakani. Put alitangaza timu ya wachezaji Alhamisi kabla ya mechi za Uganda dhidi ya Tunisia na Libya kwenye Kundi H.