UM waeleza wasiwasi juu ya hali mbaya ya usalama nchini Ethiopia

Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi mkubwa kufuatia hali mbaya ya usalama na maendeleo ya karibuni nchini Ethiopia, ikiwemo kuundwa kwa muungano mpya wa makundi yenye silaha na ripoti za kuendelea kwa mashambulio ya droni na ukosefu wa usalama.

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari, Stephane Dujarric, msemaji mkuu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amewataka wadau wote husika kujizuia kutenda ama kutoa kauli zinazoweza kufanya hali kuwa mbaya zaidi katika wakati huu wa mvutano mkubwa. Pia amewataka wadau hao kurejea tena katika majadiliano, kwani hatua za kijeshi haziwezi kutatua tofauti za kisiasa wala kushughulikia matatizo yaliyopo sasa.

NEW YORK, UNITED STATES – 2024/02/07: Secretary-General Spokesperson Stephane Dujarric attends Tor Wennesland, Special Coordinator for the Middle East Peace Process press briefing at UN Headquarters. (Photo by Lev Radin/Pacific Press/LightRocket via Getty Images)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live