Mpango wa pamoja kati ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) na jukwaa la China la kufundisha uandishi wa programu Codemao, wamechukua hatua katika kuingiza matumizi ya akili bandia (AI) kwenye shule kote Afrika.
Mtaalamu wa kitaifa wa programu katika Ofisi ya Kanda ya UNESCO kwa Afrika Mashariki Bibi Mary Nyasimi, amesema AI na zana za kidijitali zinabadilisha ufundishaji na kujifunza kote bara, zikiwapatia wanafunzi ujuzi muhimu kwa ajili ya kazi za baadaye na uvumbuzi. Akiongea kwenye mkutano uliofanyika hivi karibuni mjini Nairobi, Bibi Nyasimi amesema kuharakisha elimu ya AI ni muhimu katika kupunguza pengo la kidijitali, kuimarisha raslimali watu, na kuboresha ushindani wa kimataifa wa Kenya na bara la Afrika kwa ujumla.
