Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema linashirikiana kwa karibu na serikali ya Kenya kuimarisha hatua za udhibiti baada ya Kenya kuthibitisha mtu wa kwanza kuambukizwa Ebola, na kufariki katika hospitali moja jijini Nairobi usiku wa Jumatatu.
Taarifa iliyotolewa na WHO mjini Nairobi inasema serikali ya Kenya inaimarisha mwitikio huku ikifuatilia na kuorodhesha watu waliokaribiana na mtu huyo ili kuimarisha ufuatiliaji. Upimaji katika maeneo yenye hatari kubwa ya kuingia Kenya, mawasiliano ya wazi kuhusu hatari, na ushirikishwaji wa jamii ndiyo nguzo kuu ya mwitikio huo, ilisema.
Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Bw. Mohamed Janabi, amesema Kenya imeweka hatua muhimu za kudhibiti mlipuko na kwamba kipaumbele kwa sasa ni kuchukua hatua za haraka kubaini maambukizi mengine kabla virusi hivyo havijaenea zaidi.
“Tunaziunga mkono juhudi zinazoendelea kuimarisha mwitikio, na kwa hatua za haraka na zilizoratibiwa, tunaweza kuzuia virusi hivyo kushika kasi na kuzuia uwezekano wa mlipuko mkubwa zaidi,” alisema Janabi.
