Rais wa Ethiopia akadiria ukuaji wa 10.1% wa uchumi wa Ethiopia kwa mwaka huu wa fedha

Rais Taye Atske Selassie wa Ethiopia amesema uchumi wa Ethiopia unatarajiwa kukua kwa asilimia 10.1 katika mwaka wa fedha wa 2026/2027.

Rais Selassie ametoa kauli hiyo mjini Addis Ababa wakati akiainisha malengo makuu ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ya nchi hiyo kwenye mkutano wa pamoja wa ufunguzi wa Baraza la Wawakilishi la Umma na Baraza la Shirikisho — ambayo ni mabaraza ya bunge la nchi hiyo.

Amesema kudumisha maendeleo ya uchumi jumuishi, kutoa huduma bora za umma, kuhakikisha amani na usalama, kuboresha uratibu wa kitaasisi na kuimarisha uhusiano wa kimataifa kama vipaumbele muhimu kwa mwaka huu wa bajeti.

Kutokana na ukuaji wa uchumi wa asilimia 10.2 kwa mwaka jana, amesema juhudi za kina zinaendelea ili kudumisha kasi hiyo chanya na kufikia ukuaji wa asilimia 10.1 mwaka huu wa fedha, licha ya changamoto za ndani na kimataifa.

CopyRight : F. van den Bergh

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live