Meli ya matibabu ya Jeshi la Majini la Watu wa China, Auspicious Ark, imewasili Lome, mji mkuu wa Togo, jumapili iliyopita kuanza ziara ya kirafiki na kutoa huduma za matibabu, ikiwa ni ziara ya kwanza ya meli hiyo nchini Togo.
Wakati wa ziara hiyo, meli hiyo inayotekeleza Jukumu la Masikilizano 2026, itatoa huduma za matibabu kwa wakazi wa huko ndani ya meli, huku timu za matibabu zikitembelea hospitali ya jeshi la Togo kwa mabadilishano ya kitaaluma.
Jukumu hilo pia litahusisha matembezi ndani ya meli na mechi ya kirafiki ya mpira wa kikapu na maofisa wa jeshi la Togo ili kuimarisha zaidi mabadilishano na urafiki.
