Tarehe 2 Novemba, mashine ya kuchimba ya Israel inaonekana ikibomoa nyumba katika mji wa Zawtar al-Sharqiya, karibu na kijiji cha Zawtar al-Garbiya nchini Lebanon.
Tangu kuanza kwa vita dhidi ya kundi la Hezbollah la Lebanon, Israel imekalia maeneo mengi kusini mwa Lebanon. Chini ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande hizo mbili, Jeshi la Lebanon lilitazamiwa kuchukua udhibiti wa eneo hilo hatua kwa hatua. Makubaliano hayo yanalitaka kundi la Hezbollah, linaloungwa mkono na Iran, kuweka chini silaha, na kwamba Israel lazima iondoke nchini Lebanon; hata hivyo, maendeleo yamekuwa ya polepole. Israel imeonya kuwa itaendelea kuwepo katika eneo hilo kadri maadui zake wanavyoendelea kuwa tishio.
