Afrika yatakiwa kutumia madini ya kijani kwa ajili ya maendeleo ya viwanda

Wataalamu na watunga sera barani Afrika wametoa wito wa uhamasishaji wa rasilimali za ndani na uwezo wa viwanda ili kubadili utajiri wa madini ya kijani katika bara hilo kuwa manufaa ya kiuchumi.

Wito huo umetolewa wakati wa Kongamano la Madini ya Kijani Afrika lililomalizika Jumatano wiki hii katika Kituo cha Mikutano cha Umoja wa Mataifa Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, lililolenga kutumia madini ya kijani, kuboresha mnyororo wa thamani wa kikanda na kuongeza kasi ya maendeleo shirikishi na endelevu ya viwanda barani Afrika.

Kongamano hilo la siku tatu lililoandaliwa na Tume ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA), limekutanisha maofisa wa serikali na Umoja wa Mataifa, wataalamu wa viwanda na viongozi wa sekta binafsi ili kutafiti jinsi rasilimali za madini Afrika zinavyoweza kusaidia kuongeza thamani zaidi, kuwa na viwanda vyenye nguvu zaidi, kuratibu sera, na kuhimiza maendeleo endelevu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live