Rais wa Botswana Duma Boko ametoa wito wa kuimarisha uongozi wa kisiasa, ufadhili endelevu na ushirikiano wa kikanda ili kuongeza kasi ya kutokomeza malaria barani Afrika.
Akizungumza katika Mdahalo wa Ngazi ya Juu kuhusu Kutokomeza Malaria uliofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Gaborone, rais Boko ameeleza hali ya wasiwasi kufuatia kuibuka tena kwa ugonjwa wa malaria nchini Botswana, huku kesi zikiongezeka kutoka 290 mwaka 2024 hadi 2,451 mwaka 2025, pamoja na kuongezeka kwa vifo vinavyotokana na ugonjwa huo kutoka vifo viwili hadi 16.
Amesisitiza umuhimu wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Malaria wa Botswana wa mwaka 2025-2029, ambao unatoa kipaumbele kwa ufuatiliaji, udhibiti wa maambukizi, utambuzi wa wakati na tiba, ushiriki wa jamii na uratibu wa kuvuka mpaka.
