
Taarifa rasmi kutoka bunge la Algeria imesema wabunge wa Algeria jana waliidhinisha kutumwa kwa vikosi vya Jeshi nchini Niger.
Mkutano wa mabaraza yote ya bunge la nchi hiyo umeidhinisha taarifa iliyowasilishwa na rais Abdelmadjid Tebboune kwa mujibu wa Kifungu cha 91 cha Katiba ya Algeria.
Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa Algeria kutuma jeshi nje ya nchi tangu vita ya waarabu na Israel ya mwaka 1973.
Mapema mwezi huu, Algeria na Niger zilisaini makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi yanayolenga kuimarisha uhusiano wa kijeshi na usalama wa pande mbili wakati wa ziara ya waziri wa ulinzi wa Niger Bw. Salifou Mody huko Algiers.