DR Congo na Rwanda zarejea Geneva kwa mazungumzo ya amani

Maafisa kutoka Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wamekutana Geneva tarehe 16 na 17 mwezi Septemba, wakishiriki kwenye kikao cha saba cha Mfumo wa Pamoja wa Uratibu wa Usalama (JSCM), huku nchi hizo mbili zikitafuta kuendeleza utekelezaji wa makubaliano yao ya amani yanayoungwa mkono na Marekani.

Mazungumzo hayo yamewaleta pamoja wawakilishi wa Rwanda na DRC, huku Marekani, Qatar, Togo na Tume ya Umoja wa Afrika zikiunga mkono mchakato huo.

JSCM ilianzishwa ili kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa ahadi za usalama zilizokubaliwa na nchi hizo mbili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live