Joto kali barani Ulaya lasababisha vifo 50,000



Utafiti mpya umebaini kuwa joto kali barani Ulaya katika majira ya joto yaliyomalizika hivi karibuni limesababisha vifo vya zaidi ya watu 50,000, huku karibu theluthi mbili ya vifo hivyo ikihusishwa na mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na shughuli za binadamu.

Kwa maujibu wa matokeo ya utafiti utakaochapishwa kwenye toleo lijalo la jarida la “Nature Health”, watafiti walichunguza vifo vinavyotokana na joto kwa makundi mbalimbali ya umri katika miji 854 ya Ulaya wakati wa vipindi vya joto kali vilivyojirudiarudia mwezi Juni, Julai, na Agosti. Waligundua kuwa watu 50,391 walifariki kutokana na viwango vya juu vya joto; kati ya vifo hivyo, 32,619 vilitokana na joto la ziada lililosababishwa na uchomaji wa makaa ya mawe, mafuta, na gesi.

Watafiti hao ambao mapema mwezi huu walitoa utafiti unaofuatilia vifo vya kila mwaka vinavyotokana na joto wakati wa majira ya joto katika miji hiyo ya Ulaya, wanasema idadi hii inayochukua asilimia 71 ni kubwa kuliko ile ya majira ya joto yaliyokuwa mabaya zaidi hapo awali, ambapo watu 29,480 walifariki mwaka 2022. Waandishi wa utafiti huo wanasema kuwa takwimu za idadi ya vifo msimu huu ni ndogo kuliko uhalisia, kwani hazijajumuisha wimbi la joto kali lililotokea mwezi Mei, na zinazingatia tu vifo katika miji hiyo 854, ambayo inawakilisha takriban asilimia 40 ya watu wote barani Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live