Magari ya chapa 20 za China yaonyeshwa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Magari ya Paris

Maonyesho ya 91 ya Magari ya Paris yamefunguliwa rasmi tarehe 12 Oktoba. Kwa mujibu wa vyombo vingi vya habari vya Ufaransa, maonyesho ya mwaka huu yanashuhudia rekodi mpya ya idadi ya chapa 20 za magari za China ambayo imezidi idadi ya jumla ya kampuni za magari kutoka Ujerumani na Ufaransa.

Tovuti ya Yahoo Finance ya Marekani imesema kwamba Maonyesho hayo yamekuwa jukwaa la watengenezaji wa magari wa Ulaya kuonyesha bidhaa zao mpya, lakini mwaka huu kampuni za magari za China zimekuwa wahusika wakuu. Wakati asilimia ya magari ya nishati mpya katika soko la magari mapya la Ulaya inapopanda, uchunguzi wa sekta unaonyesha kwamba watumiaji wa Ulaya wana mtazamo mpya kuhusu thamani ya chapa za bidhaa “zinazotengenezwa na China”.

Utabiri uliotolewa na kampuni ya JPMorgan katika nusu ya kwanza ya mwaka huu unaonyesha kwamba ifikapo mwaka 2028, chapa za magari za China zinatarajiwa kuchukua asilimia 20 ya soko la Ulaya Magharibi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live