
Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda imesema kuwa mji wa Mbale mashariki mwa Uganda na mji wa Guiyang kusini magharibi mwa China imesaini barua ya nia ya kuanzisha uhusiano wa mawasiliano ya kirafiki na ushirikiano, na kuweka msingi wa ushirikiano wa siku zijazo kati ya miji rafiki.
Makubaliano hayo yaliyosainiwa jana na meya wa mji wa Mbale Joyce Matuka Kidulu na mwenzake wa Guiyang Wang Hong mjini Guiyang, yanataja sekta tano za kipaumbele kwenye ushirikiano huo zikiwemo maendeleo ya mji ya kisasa na utawala wa kidijitali, maendeleo ya kiviwanda na uwekezaji, kilimo na kuongeza thamani, utalii na mawasiliano ya kitamaduni, na uendelevu wa mazingira.
Miji hiyo miwili imekubaliana kuanzisha kikundi cha kazi cha pamoja ndani ya miezi miwili na kupanga ziara ya kiufundi huko Mbale ili kuchunguza fursa za uwekezaji katika maendeleo ya kiviwanda, usindikaji wa kahawa na utalii.