Mkutano wa siku nne wa Dunia wa Uzalishaji Viwandani wa 2026 umefunguliwa katika Kituo cha Kimataifa cha Maonyesho cha Binhu mkoani Hefei nchini China.
Mkutano huu ukiwa na kaulimbiu ya “Uzalishaji wa Akili Bandia Duniani: Kuunda Maisha Bora,” unazingatia tasnia mpya kama magari ya nishati mpya yanayounganishwa na mtandao wa akili bandia, teknolojia mpya ya habari,akili bandia, pamoja na tasnia za siku zijazo kama teknolojia ya kwantamu, roboti na uzalishaji wa kibaiolojia.
Maonyesho hayo yalivutia watazamaji wengi, ambapo wageni kutoka nchi za nje walipata uzoefu wa kutumia moduli ya mfano, pamoja na kujionea satelite ya kwanza ya China inayounganisha simu moja kwa moja na bidhaa za teknolojia ya juu kama pikipiki za Kampuni ya Chery.
