
Rais wa FIFA Fianni Infantino (mbele)
Rais wa UEFA Aleksander Ceferin amesema hatagombea dhidi ya Rais wa FIFA Gianni Infantino lakini alimwonya kiongozi huyo wa soka duniani kwamba lazima ajiuzulu vinginevyo akubali kwenda kwenye uchaguzi mwezi Machi. Infantino amekuwa chini ya shinikizo kubwa la kujiuzulu kutokana na mpango wake, ambao sasa ameutupilia mbali, wa kuuza hisa katika mashindano makubwa zaidi ya soka, Kombe la Dunia, kwa wawekezaji binafsi. Mashirikisho matatu ya soka ya bara yanamtuhumu kwa “udanganyifu” na shirika la soka la Ulaya UEFA lilitishia kususia mashindano ya FIFA. Ceferin alisema havutiwi kugombea kwa sababu mbili, kwanza anaipenda UEFA na anapenda kufanya kazi katika shirikisho hilo la soka, na pili ni kwamba, ataaminiwa zaidi kama hatavutiwa kuwania nafasi hiyo.