Wakimbizi wa Ethiopia wakimbilia mji wa mpakani kukimbia vurugu

Wakimbizi kutoka Ethiopia wamepata hifadhi katika shule zilizotelekezwa katika mji wa mpakani wa Moyale, kaskazini mwa Kenya, wakisubiri msaada wa matibabu Alhamis iliyopita.

Maelfu ya raia wa Ethiopia wamekimbilia kaskazini mwa Kenya tangu mapigano yalipozuka tarehe 18 Oktoba kati ya jamii za Waoromo na Wasomali kusini mwa Ethiopia.

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limeonya kwamba zaidi ya watu 50,000 wamekimbilia mjini humo, hali iliyoongeza shinikizo kwa matumizi ya rasilimali za eneo hilo, na watu wengine 12,000 wanahitaji hifadhi ya dharura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live