
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeitisha mkutano wa dharura tarehe 18 mwezi huu, ambapo mkurugenzi mkuu Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema janga la Ebola linaenea kwa kasi, na bado kuna hatari kubwa ya kuzidi kuenea ndani na nje ya nchi. Janga hilo limekuwa mlipuko wa pili kwa ukubwa katika historia ya majanga ya ugonjwa huo, na kasi ya kuenea kwake ni kubwa zaidi kuliko milipuko yote iliyopita. Amesema,kudhibiti ugonjwa bado kunahitaji kuharakisha mabadilishano ya data, kuimarisha ufuatiliaji, kuendelea kutoa fedha, na kuimarisha uratibu wa kuvuka mipaka.
Bw. Tedros amesema hadi sasa, karibu watu 5,000 wameambukizwa na zaidi ya 2,300 wamefariki, ugonjwa umeenea hadi maeneo mengi ya DRC, na bado haujadhibitiwa ambapo kuna minyororo ya maambukizi ambayo bado haijagunduliwa. Kwa sasa, chanjo mbili zilizotolewa mahsusi kwa ajili ya virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo, zimeingia katika kipindi cha majaribio kwa binadamu, na chanjo nyingine imeonyesha kinga (cross protection) katika majaribio kwa wanyama.