
Rais wa Kenya William Ruto amepongeza hatua ya kuichagua Nairobi kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Riadha ya Dunia ya 2029 akisema huo ni wakati wa kihistoria kwa Kenya na Afrika.
Kenya itakuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Riadha ya Dunia, ambalo ni tukio kuu la kimataifa la mchezo huo wa riadha.
Uamuzi huo ulifanywa wakati wa Mkutano wa 242 wa Baraza la Riadha la Dunia uliofanyika tarehe 14 na 15 huko Budapest, kufuatia mchakato wa ushindani wa zabuni uliohusisha pia London, Roma na Munich.