Mkutano wa Kilele wa Haidrojeni ya Kijani wa Afrika wafunguliwa huko Cape Town

Mkutano wa Kilele wa Haidrojeni ya Kijani Afrika wa 2026 umefunguliwa mjiniCape Town, ambapo Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametoa wito wa kuharakisha utekelezaji na kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji, ili kuubadilisha uwezekano wa haidrojeni ya kijani barani Afrika uwe ukuaji wa viwanda, usalama wa nishati, na maendeleo endelevu.

Mkutano huo wa siku mbili umeshirikisha wajumbe zaidi ya elfu moja kutoka nchi 17, wakiwemo maofisa wa serikali, wawekezaji, wataalamu wa nishati na viongozi wa sekta hiyo.

Kwenye hotuba iliyotolewa kwa niaba ya rais Ramaphosa, Waziri wa Umeme na Nishati Kgosientsho Ramokgopa amesema, Afrika imejiweka kwenye nafasi ya kuwa kituo kikuu duniani cha haidrojeni ya kijani ikitaja nishati zake nyingi mpya, maliasili ya maji, pamoja akiba kubwa ya madini muhimu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live