
Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema, ndege ya kijeshi ya aina ya An-12 ilianguka jana kwenye eneo la Kemerovo, na watu wote 19 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo wamefariki.
Wizara hiyo imeongeza kuwa ndege hiyo ilianguka katika eneo lisilokaliwa na watu.
Wizara hiyo pia imesema uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya kiufundi. Kamati kutoka Jeshi la Anga la Russia inafanya kazi katika eneo la ajali ili kubaini mazingira kamili ya tukio hilo.