Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema masuala yote katika kanda hiyo, kuanzia hali ya mvutano, kupamba moto kwa mapigano na hadi msukosuko katika mlangobahari wa Hormuz, yanasababishwa na uvamizi wa Marekani. Marekani haiwezi kuongeza vikwazo na shinikizo dhidi ya Iran kwa upande mmoja, huku ikidai kuwa inataka kufanya mazungumzo nayo.
Amesema Iran inapenda kufanya mazungumzo tangu zamani hadi sasa, lakini lazima Marekani iondoe kwanza tishio na vikwazo. Amesema kama kweli Wamarekani wanatafuta mazungumzo na makubaliano, vitendo vyao vya sasa vinakinzana na hoja zao, na havina mantiki yoyote.
Rais Pezeshkian amesisitiza kuwa Marekani haiwezi kutimiza malengo yake kwa njia ya vita, bali inaweza kusababisha uharibifu na hasara tu, sio tu kwa Iran, bali pia kwa kanda nzima.
