
Rais wa China Xi Jinping ametaka juhudi zaidi katika kutafiti na kutekeleza mwongozo wa kanuni za kikao cha tano cha Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na kutafuta matokeo mapya katika maendeleo ya ubora wa juu ya Eneo la Ghuba Kuu la Guangdong-Hong Kong-Macao.
Rais Xi amesema hayo wakati wa ziara ya ukaguzi huko Zhongshan, mkoa wa Guangdong, kusini mwa China. Akisisitiza utekelezaji kamili na wa uaminifu wa maamuzi na mipango iliyotolewa katika kikao hicho na kutumia maendeleo mapya katika kudumisha kikamilifu uongozi wa Chama, rais Xi ametaka kazi nzuri zaidi ifanyike katika kuendeleza maingiliano ya maendeleo kando ya Mlango wa Mto Pearl.
Amesema ujenzi wa Eneo la Ghuba Kuu ni mpango muhimu wa kimkakati uliotolewa na Kamati Kuu ya CPC, na kuitaka miji kado ya Mlango wa Mto Pearl ikiwemo Guangzhou, Shenzhen, Zhuhai, Dongguan na Zhongshan kuchukua nafasi ya uongozi.