Wizara ya Mambo ya Nje ya China: China na India zinapaswa kuwa washirika

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema, rais Xi Jinping wa China na waziri mkuu wa India Bw. Narendra Modi wamekubaliana kwamba, China na India zinapaswa kuwa washirika, ambayo ni makubaliano muhimu zaidi kati ya viongozi hao wawili kuyafikia wakati wa mkutano wa 18 wa wakuu wa nchi za BRICS mjini New Delhi.

Viongozi hao wawili wamekubaliana kuwa, China na India, zikiwa nchi mbili zenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani na wanachama muhimu wa Nchi za Kusini, zinapaswa kuzingatia maendeleo kama sehemu kuu ya pamoja, kuimarisha mawasiliano ya kirafiki na ushirikiano wa kunufaishana, kuboresha mtazamo wa watu kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kuhimiza maendeleo mazuri na tulivu ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara.

Pande zote mbili zimekubali kuungana mkono kwenye suala la uenyekiti wa BRICS, kuhimiza ushirikiano wa Nchi za Kusini, kuendeleza mfumo wa dunia ya ncha nyingi na kufanya kazi kama nguvu ya utulivu na maendeleo katika dunia yenye machafuko.

China itachukua uenyekiti wa BRICS na kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 19 wa wakuu wa BRICS mwaka ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live