
Dolly Parton, msanii maarufu wa muziki wa country ambaye sauti yake ya mtetemo, uandishi wa nyimbo zenye kugusa moyo na mavazi yake ya kung’aa yaliyomfanya ainuke kutoka chini hadi kuwa nyota maarufu duniani, amefariki dunia Jumanne huko Nashville, Tennessee, Marekani, akiwa na umri wa miaka 80. Hata hivyo chanzo cha kifo hakikufichuliwa.
Parton Aliandika mamia ya nyimbo, ikiwa ni pamoja na nyimbo za kitambo kama “Jolene,” “Coat of Many Colors” na “I Will Always Love You,” ambazo zilifikia mauzo ya zaidi ya milioni 100 duniani kote na zaidi ya stream bilioni 1 mtandaoni. Parton, ambaye alipiga ala kama vile banjo, gitaa na dulcimers kwa kutumia kucha zake ndefu wakati wa maonesho, alikuwa mfadhili mkarimu na mfanyabiashara aliyefanikiwa ambaye miradi yake ilijumuisha viwanja vya kufurahia (theme park) chini ya Mlima wa Smoky karibu na mahali alipozaliwa.
Bendera za Marekani zinapepea nusu mlingoti kwenye Mnara wa Washington ili kuomboleza kifo chake. Rais wa Marekani Donald Trump aliamuru bendera hizo kupeperushwa nusu mlingoti kwa wiki moja.