
Mtaalamu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bi. Marie Roseline Belizaire jana kwenye mkutano wa mtandaoni wa Ofisi ya Kanda ya Afrika ya WHO amesema, ingawa kasi ya kuenea kwa Ebola imepungua katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), lakini kiwango cha janga nchini humo bado hakijaanza kushuka.
Bi. Belizaire amesema, kufikia Jumatatu, DRC ilikuwa imerekodi wagonjwa 5,656 waliothibitishwa na vifo 2,715, na hivyo kufanya kiwango cha vifo kuwa asilimia 48.
Wakati huo huo, Bi. Belizaire ametangaza kumalizika kwa mlipuko wa hivi karibuni wa Ebola nchini Uganda, baada ya nchi hiyo kukaa siku 42 mfululizo bila kuripoti mgonjwa mpya aliyethibitishwa.