Kampuni za Sharpa na DQ zashirikiana kuanzisha mkahawa wa ice cream unaoendeshwa na roboti

Mkahawa wa kwanza wa ice cream unaoendeshwa na roboti ulioanzishwa kwa ushirikiano wa kampuni maarufu ya ice cream Dairy Queen na kampuni ya roboti za AI ya Sharpa, umefunguliwa rasmi Agosti 29, 2026, katika Mtaa wa Wujiang, mjini Shanghai,China.

Habari zinasema, mkahawa huo ni wa kwanza unaojiendesha kikamilifu, na unaofanya kazi mwaka mzima bila mapumziko. Kwa mara ya kwanza, roboti za kampuni ya Sharpa zimefanikiwa kukamilisha kazi nzima katika mazingira halisi ya kibiashara ya kujiendesha kikamilifu, na zinaweza kutimiza hatua 55 zinazofuatana kuanzia kuagiza, kutengeneza, hadi kuwasilisha ice cream ya ‘Blizzard’ kwa wateja,na pia zinaweza kufanya kazi kila siku kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nne usiku bila ya kupumzika kwa mwaka mzima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live