Teknolojia ya AI ya China yapata umaarufu nchini Kenya

Miundo ya Akili Bandia ya China (Al) inapata umaarufu miongoni mwa waendelezaji programu na makampuni ya teknolojia ya Kenya kutokana na sifa zake za gharama nafuu, utendaji wenye ushindani na kuwa Chanzo Huria,  ikitoa chaguo la kuvutia kwa soko linalohitaji masuluhisho ya Akili Bandia yenye gharama nafuu na yanayokidhi mahitaji ya kienyeji.

Uchambuzi wa hivi karibuni uliofanywa na gazeti la The New York Times umeonyesha kuwa miundo ya China ya Akili Bandia imechangia takriban nusu ya matumizi ya Akili Bandia kwenye OpenRouter, jukwaa linalotoa takriban miundo 400 ya Akili Bandia, ikipanda kutoka chini ya asilimia 25 katika mwaka uliopita.

Waendelezaji programu na makampuni ya teknolojia nchini Kenya yanazidi kutumia miundo ya China ya Akili Bandia kama vile DeepSeek na Qwen kwa matumizi kuanzia teknolojia ya kisheria na ushauri wa kibiashara, hadi uchakataji wa hati na usanidi wa programu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live