Watu 21 wafariki, 541 hawajulikani walipo baada ya maporomoko ya matope kuikumba forodha ya mpakani mkoani Xizang, China

Watu 21 wamethibitishwa kufariki na wengine 541 bado hawajulikani walipo hadi kufikia Jumatano mchana baada ya maporomoko ya matope kuikumba forodha ya Gyirong kwenye mpaka wa China na Nepal kusini magharibi mwa Mkoa wa Xizang Agosti 26.

Habari zinasema waokoaji wamerejesha vipande 847 vya mali binafsi, mamlaka za mitaa zimepokea simu 876 kutoka kwa jamaa za wahanga na watu waliopotea, na wamekuwa wakiitikia maombi yao kwa haraka.

Maporomoko hayo yalisababishwa na kumeguka kwa pande kubwa la barafu, ni maporomoko makubwa ya matope yaliyolikumba eneo hilo na kuharibu majengo, vifaa vya umeme na sehemu ya barabara kuu inayoelekea kwenye forodha ya Gyirong.

Licha ya hali ngumu, China imetuma mara moja helikopta, boti za mwendo kasi na rafu za mpira ili kuwafikisha waokoaji kwenye forodha iliyoathiriwa na maporomoko hayo. Timu za uokoaji ardhini zimetumia saa 12 kupita katika barabara zenye miteremko mikali na kufika kwa mguu kwenye eneo la tukio.

default

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live