Wake wa marais wa China na Marekani watembelea Jumba la Makumbusho ya Kitaifa ya Sanaa za Asia

Asubuhi ya Septemba 24, mke wa Rais wa China Bibi Peng Liyuan na mke wa Rais wa Marekani Bibi Melania Trump, walitembelea kwa pamoja Jumba la Makumbusho ya Kitaifa ya Sanaa za Asia mjini Washington.

Wake hao wawili wa marais walitembelea kumbi kadhaa ikiwemo ukumbi wa tausi. Bibi Peng Liyuan ameisifu Marekani kwa kurejesha vitu vya kale vya China mara nyingi katika miaka ya karibuni, na pia ameeleza matumaini yake kuwa China na Marekani zitaendelea kuimarisha mawasiliano ya kiutamaduni na ushirikiano katika uhifadhi wa urithi wa kiutamaduni, ili kuzidisha urafiki kati ya watu wa nchi hizi mbili.

Baada ya kutembelea makumbusho hayo, Bibi Peng Liyuan na Bibi Melania Trump walitazama kwa pamoja vijana wa Marekani wakiimba nyimbo za Kichina, na kuzungumza nao. Bibi Peng amewahamasisha vijana hao kuendelea kujifunza lugha ya Kichina na utamaduni wa China, na kuwa mabalozi wa urafiki kati ya China na Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live