Meneja kitengo cha Huduma za Hali ya Hewa na Matumizi katika Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Rwanda, Anthony Twahirwa amesema, nchi hiyo inaimarisha utayari wake kwa matukio ya hali mbaya zaidi ya hewa inayotokana na El Nino, ambayo imetabiriwa kuathiri kanda hiyo.
Kwa mujibu wa mtazamo wa hali ya hewa wa kikanda uliotolewa na Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa na Matumizi (CPAC) cha Mamlaka ya Kiserikali ya Maendeleo ya nchi za Afrika Mashariki (IGAD) uliotolewa mwezi Agosti, sehemu nyingi za Pembe Kuu ya Afrika zinatabiriwa kukumbwa na hali mbaya ya hewa ya El Nino na mvua kubwa kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba.
Katika mahojiano hivi karibuni na Shirika la Habari la China, Xinhua, Twahirwa amesema wakati mvua zinazotarajiwa zinaweza kuwa na faida kwa kilimo na kuongeza vyanzo vya maji, pia zinaweza kuleta hatari ya mafuriko, maporomoko ya ardhi, mmomonyoko wa udongo na kuharibu miundombinu, na hivyo kuathiri maisha ya watu na shughuli za kiuchumi.
