Wataalamu wamesema, ahadi ya China ya kufungua chanzo, uwazi, ushirikiano na kushirikishana inatoa njia ya kivitendo kwa nchi za Dunia ya Kusini kutumia fursa zinazopatikana kutokana na maendeleo ya Akili Bandia (AI) na kuziba pengo llinaloletwa na AI kati ya Kaskazini na Kusini.
Katika Jukwaa la Usasa wa Dunia ya Kusini la mwaka 2026 lililofanyika jumatano wiki hii katika mji mkuu wa Misri, Cairo, washiriki wamesema usasa katika Dunia ya Kusini uko katika kipindi muhimu cha kukabiliana na vikwazo vya maendeleo, kuondoa pengo la uwezo na kuleta mageuzi katika vichocheo vya ukuaji, na kusisitiza haja ya kutumia vizuri AI kuimarisha kasi ya maendeleo ya nchi husika.
Wataalamu na wasomi wamesema nchi za Dunia ya Kusini zinapaswa kuchukua nafasi zaidi katika majadiliano na ushirikiano kuhusu maadili ya AI, usalama, usimamizi wa takwimu na kuweka vigezo, na kwa njia hiyo kuboresha mfumo jumuishi wa kimataifa wa kusimamia AI.
