Viongozi wa Afrika wahimiza hatua za pamoja na kujitegemea kwenye mikutano nchini Misri

Viongozi wa Afrika wamehimiza hatua za pamoja na kujitegemea kwa ajili ya kutatua changamoto za pamoja na kukuza maendeleo endelevu barani humo kwenye mikutano ya ngazi ya juu iliyofanyika huko New Alamein nchini Misri kuanzia tarehe 2 hadi 4 mwezi Oktoba.

Mikutano hiyo ni pamoja na Kongamano la Afrika la Alamein, Mkutano wa 8 wa Kati ya Mwaka wa Uratibu kati ya Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kiuchumi za Kikanda.

Akihutubia ufunguzi wa mkutano wa uratibu wa Umoja wa Afrika, Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi amesisitiza tena msimamo wa Misri wa kupinga uingiliaji wa nje katika mambo ya ndani ya nchi za Afrika na kutoa wito wa kuwe na heshima kwa mamlaka, umoja na ukamilifu wa ardhi wa nchi hizo. Rais El-Sisi amesisitiza umuhimu wa kutatua masuala yanayovuka mipaka ya nchi kupitia ushirikiano na mazungumzo, ikiwemo usimamizi na matumizi ya maliasili na mito inayovuka mipaka ya nchi kwa mujibu wa sheria ya kimataifa.

African road networks. Earth globe and map, centred on Africa, showing the populated areas (yellow) that have a paved road network. In 2013, it was estimated that around 70 percent of Africa’s roads are unpaved, with many of the paved roads being in poor condition.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live