Naibu Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ina wasiwasi mkubwa kutokana na vurugu zinazoendelea, ongezeko la idadi ya watu waliokimbia makazi na kuzorota kwa hali ya usalama wa chakula nchini Sudan.
Haq amesema hayo Jumatatu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York.
Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yaliyotokea hivi karibuni katika sehemu mbalimbali nchini Sudan si kama tu yamesababisha vifo na majeruhi kwa raia, bali pia yamevuruga shughuli za utoaji wa misaada ya kibinadamu nchini humo.
Haq pia amesisitiza kuwa, ukosefu wa fedha za msaada umezidisha msukosuko wa kibinadamu nchini Sudan, na mashirika ya misaada yamelazimika kupunguza msaada na kusababisha idadi kubwa ya watu kukabiliwa na hatari ya kukosa msaada wa chakula.
