WHO yaonya kuwa mapigano mapya yanasababisha hali mbaya ya mfumo wa afya kaskazini mwa Ethiopia

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuwa, hospitali katika kanda ya kaskazini nchini Ethiopia zinakabiliwa na uhaba wa wahudumu wa afya, dawa na vifaa, wakati mapigano mapya na mashambulio ya droni yakivuruga huduma za afya.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dr. Tedros Ghebreyesus amesema, hali mbaya ya usalama pia inazuia operesheni za magari ya wagonjwa na kuzuia upelekaji wa vifaa muhimu vya afya katika baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa.

Onyo hilo limekuja baada ya mashambulio ya droni katika mikoa ya Amhara na Tigray mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo raia wengi waliuawa kufuatia mashambulio hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live