Abiy Ahmed ateuliwa tena kuwa waziri mkuu wa Ethiopia

Bunge la Serikali ya Shirikisho ya Ethiopia Oktoba 5 lilikutana kuunda serikali mpya na kupitisha uteuzi wa Abiy Ahmed kuwa waziri mkuu wa serikali mpya. Bw. Abiy Ahmed aliapishwa rasmi bungeni kushika wadhifa huo.

Katika uchaguzi wa wabunge uliofanyika Juni mwaka huu, Chama cha Prosperity Party (PP) kilipata ushindi na kunyakua viti 438 kati ya vyote 486 vya Bunge. Mwenyekiti wa Chama cha PP Abiy Ahmed Aliteuliwa kuwa mgombea wa waziri mkuu wa serikali mpya.

Bw. Abiy Ahmed amekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo mwezi Aprili mwaka 2018, na aliendelea kwa muhula wa pili kuanzia mwaka 2021.

Prime Minister of Ethiopia Abiy Ahmed Ali attends the BRICS Summit in New Delhi, India, Saturday, Sept. 12, 2026. (Alexander Kazakov, Sputnik, Kremlin/Pool Photo via AP)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live