Afisa wa UM atembelea DRC kutathmini mwitikio wa janga la Ebola

Ofisi ya Uratibu wa Mambo ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema janga la Ebola linaloendelea kuenea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) limesababisha vifo zaidi ya 3,200. Mratibu wa OCHA Bw. Damien Mama ameanza ziara ya yake ya siku nne katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini DRC kuanzia tarehe 8 ili kutathmini mwitikio wa janga hilo na hali ya kibinadamu katika eneo hilo.

Hivi karibuni serikali ya DRC imeshirikiana na washirika wake ikiwemo Shirika la Afya Duniani, kuanzisha awamu mpya ya mpango ya kukabiliana na Ebola, na katika miezi sita ijayo, dola za kimarekani bilioni 1.3 zitatengwa kwa ajili ya kazi za usimamizi wa maambukizi, ufuatiliaji wa waliogusana na wagonjwa, matibabu ya wagonjwa, ushiriki wa jamii na uhakikisho wa ugavi na kadhalika.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, operesheni zijazo bado zinakabiliwa na ukosefu wa fedha, ambapo mpango wa dharura wa kibinadamu unaohitaji dola za kimarekani bilioni 2.1 sasa umepata dola bilioni moja tu.

A health worker pauses after disinfecting a treatment center for Ebola patients, in Beni, North Kivu province, eastern Congo, Monday, Aug. 31, 2026. (AP Photo/Sebastien Kitsa Musayi)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

LEOFM

Maisha TV
Live
Tap to listen live