Shirika la Nchi Zinazozalisha Mafuta (OPEC) lilitoa taarifa tarehe 6 Septemba likisema nchi saba wanachama za “OPEC+” zimeamua kudumisha kiwango cha uzalishaji wa mafuta ghafi mwezi Oktoba, sawa na kilekile cha Septemba, huku zikisisitiza tena kulinda utulivu wa soko.
Wawakilishi kutoka Saudi Arabia, Russia, Iraq, Kuwait, Kazakhstan, Algeria na Oman walifanya mkutano kwa njia ya mtandao, kuchunguza hali na mustakabali wa soko la mafuta duniani. Hii ni mara ya kwanza kwa nchi hizo kusimamisha ongezeko la uzalishaji tangu walipoanza kuongeza uzalishaji mwezi Aprili mwaka huu.
Taarifa ilisema nchi hizo saba zitaendelea kutathmini hali ya soko la kimataifa la mafuta ghafi kila mwezi, na mkutano ujao umepangwa kufanyika Oktoba 4.
Wachambuzi wanasema vita ya Mashariki ya Kati imezuia usafirishaji wa mafuta kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz, na hivyo kuathiri uwezo wa “OPEC+” wa kushawishi bei ya mafuta na sehemu zao za soko. “OPEC+” itatathmini uwezo wa uzalishaji wa nchi wanachama baadaye mwaka huu, ili kuweka kiwango cha msingi cha uzalishaji kwa mwaka 2027.
